Mwili wa Liu Xiabao wachomwa

Mkewe Liu Xiabao alihudhuria mazishi yake na watu wengine Haki miliki ya picha HANDOUT
Image caption Mkewe Liu Xiabao alihudhuria mazishi yake na watu wengine

Ibada ya mazishi imefanywa kwa aliyekuwa mshindi wa tuzo la Nobel, Liu Xiabao.

Mwili wake ulichomwa katika mji wa Shenyang katika tukio lililohudhurwa na marafiki na familia, kukiwemo mkewe Liu Xia aliyekabidhiwa majivu ya mumewe.

Amekuwa akizuiliwa nyumbani kwa muda mrefu ingawa msemaji wa Jiji la Shenyang alieleza kuwa anaamini mama huyo kwa sasa yuko huru.

Liu Xiaobo alihukumiwa kifungo cha miaka 11 mwaka 2009 kwa kosa la uhaini.

Ingawa watu mashuhuri kimataifa wangali wanatuma jumbe za rambirambi vyombo vya habari va uchina vingali vinamkosoa.

Gazeti moja, The Global Times, lilidai kuwa Liu alitaka kupindua Serikali.