Mtu aliyejihami na kisu awauwa watalii Misri

Wafanyakazi wa Serikali wa Misri wanasema kuwa mtu huyo anaendelea kuhojiwa ili wajue hasa lengo lake. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafanyakazi wa Serikali wa Misri wanasema kuwa mtu huyo anaendelea kuhojiwa ili wajue hasa lengo lake.

Mwanamume mmoja aliyekuwa na kisu amewashambulia watalii wa kigeni nchini Misri katika ufuo wa mgahawa mkuu ulio kwenye ufuo wa Bahari ya Shamu ya Hurghada.

Maafisa wa Serikali na matabibu wanasema kuwa watu wawili wameuawa katika shambulio hilo ambapo watalii wengine wanne wametajwa kujeruhiwa.

Mshambulizi huyo ametiwa mbaroni.

Wafanyakazi wa Serikali wa Misri wanasema kuwa mtu huyo anaendelea kuhojiwa ili wajue hasa lengo lake.

Wizara ya Usalama wa ndani ilisema kuwa mtu huyo aliogelea hadi walikokuwa watalii kutoka ufuo uliokuwa karibu.

Mwaka uliopita, kulikuwepo na shambulio lingine Hurgada ambapo watalii wawili walijeruhiwa.

Wapiganaji Waislamu wamelenga idara ya utalii kwa miaka sasa katika juhudi za kuangamiza kiungo muhimu cha kuletea Misri Fedha za kigeni.