Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem

Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem

Wakuu wa Israel wamefungua tena eneo takatifu na tete sana, mjini Jerusalem ambalo Wayahudi wanaliita Temple Mount, na Waislamu ni al-Haram al-Sharif.

Lakini waumini wengi waislamu walikataa kuingia katika eneo hilo, kwa sababu ya hatua mpya za usalama ambazo zimewekwa na Waisraili, na sala ya mchana ilifanywa nje ya eneo hilo.

Eneo hilo lilifungwa kwa mara ya kwanza baada ya miongo mingi, siku ya Ijumaa, kufuatia ghasia karibu na eneo hilo.

Askari polisi wawili walipigwa risasi na kuuwawa na wanaume wa kiarabu wa Israel waliokuwa na silaha, ambao walifatwa na kuuliwa.

Image caption Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem

Mada zinazohusiana