Ndugu yake rais wa Iran atupwa korokoroni

Hossein Ferydoun Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hossein Ferydoun

Ndugu rais wa Iran, Hassan Rouhani, amekamatwa, huku kukiwa na madai kwamba amehusika na uhalifu wa kifedha.

Afisa mwandamizi wa mahakama, alisema Hossein Fereydoun, amechunguzwa mara kadha.

Yeye ni mshauri mkuu wa Rais Rouhani, ambaye kati ya viongozi wa Iran, ni mwenye msimamo wa wastani na wa kutaka mabadiliko.

Viongozi wasiotaka mabadiliko, wamekuwa wakidai kuwa Bwana Fereydoun afikishwe mahakamani, kutokana na kashfa inayohusu benki.

Jana alitakiwa akulipa fidia lakini kwa sababu alishindwa kulipa dhamana alipelekwaa korokooni

Bwana Ferydoun ataachiliwa mara atakapolipa dhamana hiyo.