Korea kusini kuzungumza na Kaskazini?

Korea kaskazini na maonesho ya silaha Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Korea kaskazini na maonesho ya silaha

Serikali ya korea kusini imependekeza mazungumzo ya kwanza ya kijeshi na korea kaskazini, kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2015.

Haya yanajiri baada ya korea kaskazini kufanya majaribio ya zana zake za masafa marefu.

Waziri wa ulinzi wa korea kusini, amesema utawala wa Seoul, umeitisha mkutano huo, ili kupunguza vitendo vya uhasama katika mpaka wake na Korea Kaskazini, vinavyoibua uhasama za kijeshi.