Watu 8 wauwawa kwenye mafuriko Marekani

Map
Image caption Watu 8 wauawa kwenye mafuriko Arizona Marekani

Mafuriko mabaya yaliyosabishwa na mvua kubwa yamesomba kidimbi kimoja cha kuogelea katika jimbo la Arizona nchini Marekani na kuwaua watu 8.

Takriban wawili kati ya wale waliouawa ni watoto.

Shughuli za kutafuta zinandelea kuwatafuta watu ambao bado hawajulikani waliko.

Mafuriko yalitokea eneo la Cold Springs karibu na Patson Jumamosi alasiri.

"Kundi la watu walikuwa wakistarehe eneo la chini la mto, alisema afisa wa polisi David Horning.

Mvua haikuna inayesha eneo ambapo watu walikuwa wakiogelea

Takribana watu wanne wameokolewa na sasa wanatibiwa

Mada zinazohusiana