Telegram kufunga akaunti za makundi ya ugaidi Indonesia

Telegram app on a mobile phone Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Telegram kufunga akaunti za makundi ya ugaidi Indonesia

Mtandao wa kutuma ujumbe kwa njia ya simu wa Telegram, umeahidi kuwa utafunga akaunti zinazohusiana na ugaidi, baada ya serikali ya Indonesia kufunga huduma za mtandao huo nchini humo.

Wizara ya mawasialiano na teknolojia nchini Indonesia ilifunga huduma za Telegram siku ya Ijumaa na kutishia kufunga mifumo yake yote.

Indonesia inadai kuwa Telegram imetumiwa kuunga mkono itikadi kali na kutoa maelekezo ya kufanya mashambulizi.

Mwanzilishi wa mtandao huo amesema kuwa ameghadhabishwa na hatua hiyo.

Katika taarifa Pavel Durov, alisema kuwa Telegram sasa imeondoa akaunti zote zinazohusika na ugaidi zilizotajwa na serikali.

Hatua ya serikali inakuja huku kukiwa na wasi wasi wa kuibuka kwa kundi la Islamic State kusini mashariki mwa Asia.

Kundi hilo limedai kuhusika kwenye mashambulizi kadha nchini Indonesia mwaka huu na limepigana na jeshi mjini Marawi katika kisiwa cha mindanao nchini Ufilipino.

Mada zinazohusiana