Maafisa wa Marekani na Urusi kukutana

Jengo ambalo Marekani linadai kutumiwa na Urusi kufanya uj Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jengo ambalo Marekani linadai kutumiwa na Urusi kufanya ujasusi

Maafisa Waandamizi wa Urusi na Marekani wanatarajia kufanya mazungumzo mjini Washington kwa kile kilichoonekana kama jaribio la mwisho kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili, ikiwa ni ahadi za kampeni za uchaguzi za Rais Donald Trump.

Desemba mwaka jana, utawala wa Rais aliyemaliza muda wake Barack Obama uliyafunga majengo mawili na kuwarudisha nyumbani wanadiplomasia 35 wa Urusi.

Hata hivyo Urusi ilikataa kulipiza kisasi kwa Marekani. Lakini katika siku za hivi karibuni ilitishia kuchukua hatua mpaka pale Marekani itakaporudisha vitendea kazi vya mali zake hizo.

Mwandishi wa BBC, mjini Moscow anasema Rais Trump yuko njia panda, kwani kuchukua maamuzi kwa sasa dhidi ya Urusi inaweza kuwa suala tata, kutokana na uchunguzi unaoendelea kuhusiana na uchaguzi, ambapo timu yake inadaiwa kuwa na mahusiano na Urusi katika kupata taarifa.

Lakini iwapo Urusi nayo italipiza kisasi inaweza kuvuruga matumaini yaliyobaki kwamba anaweza kuboresha mahusiano na Moscow.