Upinzani Venezuela waitisha mgomo tena

Viongozi wa Upinzania Venezuela Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Upinzania Venezuela

Upinzani nchini Venezuela wameitisha mgomo wa nchi nzima kwa saa 24, siku ya Alhamisi, ikiwa ni sehemu ya njia mpya kuongeza mbinyo kwa serikali inayoongozwa na Rais Nicolas Maduro.

Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo kupiga kura ya maoni isiyo rasmi dhidi ya mipango ya Rais Maduro kutaka kubadilisha katiba ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake, kiongozi kutoka chama cha upinzani cha National Unity Coalition Freddy Guevara amesema Wavenezuela wengi waliopiga kura, wanataka kuwepo kwa demokrasia.

Upinzani unataka Rais Maduro kusitisha uamuzi wake wa kupigia kura mabadiliko hayo ya katiba mwishoni mwa mwezi huu.