Suala la ObamaCare laibuka tena

Mgonjwa akipata huduma ya afya nchini Marekani Haki miliki ya picha Dr Van Breeding at workImage copyrightMALCOLM J WI
Image caption Mgonjwa akipata huduma ya afya nchini Marekani

Maseneta wawili zaidi wa chama cha Republican, Marekani wamesema watapinga mpango wa chama chao wa kufutilia mbali mpango wa bima ya afya ulionzisha na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Barrack Obama.

Kufuatia tangazo hilo sasa itakuwa vigumu zaidi kwa mswada huo kuidhinishwa kama ilivyo.

Mike Lee na Jerry moran, wamesema mswada wa sasa hautoshi kufutilia mbali mpango huo wa bima ya afya maarufu ObamaCare.

Wakati wa Kampeini yake Trump alihaidi kuwa atalifutilia mbali mpango huo wa Obamacare.