Miili ya watu waliotoweka mwaka 1942 yapatikana kwenye barafu Uswisi

The spot where the two bodies were found in glacier Haki miliki ya picha Télévision Suisse Romande
Image caption Bernhard Tschannen aonyeha sehemu miili hiyo ilipatikana

Kuyeyuka kwa mawe makubwa ya barafu nchini Uswisi kumefichua miili miwili inayoaminika kuwa ya mtu na mkewe waliotoweka miaka 75 iliyopita.

Marcelin na Francine Dumoulin walitoweka wakati walienda kuchunga ng'ombe wao katika milima ya Alps mwaka 1942.

Watu hao walikuwa na watoto saba.

Mtoto wao wa mwisho wa kike ambaye sasa ana umri wa 79, anasema habari hizo zimemletea utulivu na anataka kuwafanyia maziko mema.

"Tulitumia maisha yetu yote kuwatafuta," alisema Marceline Udry-Dumoulin.

Uchunguzi wa DNA unatarajiwa kufanywa.

Polisi wanasema kuwa miili hiyo iligunduliwa wiki iliyopita katika eneo la Tsanfleuron na mfanyakazi kutoka kampuni ya kuteleza kwa barafu ya Glacier 3000.

Mada zinazohusiana