Kaka wa rais wa Iran aachiliwa kwa dhamana

Hossein Ferydoun Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hossein Ferydoun aliachiliwa Jumatatu usiku baada na ripoti kuwa alilipa mamilioni ya dola, kama dhamana.

Kaka wa rais wa Iran Hassan Rouhani ameachiliwa baada ya kukamatwa baada ya kuzuiliwa na polisi kwa muda wa siku mbili.

Hossein Ferydoun aliachiliwa Jumatatu usiku baada na ripoti kuwa alilipa mamilioni ya dola, kama dhamana.

Mr Ferydoun anaaminiwa kukamatwa kuhojiwa siku ya Jumamosi kutokana na madai ya ufisadi.

Kukamatwa kwake kulionekana kama tofauti zilizopo kati ya rais na mahakama.

Haijulikani ni nini haswa kilichosababisha bwana Ferdoun kukamatwa ili kuhojiwa.

Licha ya kutokuwa na cheo rasmi serikalini, bwana Ferydoun alikuwa msaidizi wa karibu wa bwana Rouhani wakati wa muhula wake wa kwanza ofisini akishiriki katika mazungumzo na mataifa yadunia kuhusu mpango wa nuklia wa Iran.

Mada zinazohusiana