Marekani yaiwekea Iran vikwazo vipya

File photo, released by semi-official Iranian Students News Agency, of a long-range S-200 missile fired in a military drill in the port city of Bushehr

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Marekani imetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Iran, kuhusiana na mpango wake wa silaha zake za kinuklia

Marekani imetangaza vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Iran, kuhusiana na mpango wake wa silaha zake za kinuklia.

Marekani inasema kuwa, inawalenga pia baadhi ya watu mashuhuri au rasilimali, ambazo zinaunga mkono mpango huo wa silaha za kinuklia mbali na kikosi cha ulinzi chenye nguvu nyingi nchini Iran cha Republican Guards.

Hatua hiyo inatangazwa siku moja tu baada ya Ikulu ya White House kusema kuwa Iran imeanza kutekeleza mpango wa silaha za nuklia.

Taarifa hiyo pia ilikosoa hatua ya Iran ya kuunga mkono serikali ya Syria na makundi kama Hezbollah na Hamas.

Marekani ina wasi wasi kufuatia shughuli za Iran eneo la mashariki ya kati, zinazovuruga utulivu wa eneo hilo.

Pia iliilaumu Iran kwa kuendeleka mzozo ulio nchini Yemen kwa kuunga mkono waasi wa Houthi. Iran bado haijatamka lolote kufuatia hatua hizo za hivi punde.