Trump na Putin walifanya kikao cha siri G20

Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa pili wa siri
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa pili wa siri

Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin katika mkutano wa pili wa siri ambao haukutajwa ulipofanyika katika kikao cha mkutano wa mataifa ya G20, imebainika.

Walifanya mazungumzo baada ya mkutano wao wa kwanza lakini ukulu ya White House haijatoa maelezo kuhusu kile kilichozungumziwa.

Rais Trump amekana madai ya kufanyika kwa mkutano huo wa siri na Putin na kusema ni ''habari bandia''.

Uhusiano wa viongozi hao wawili unachunguzwa kufuatia madai kwamba kampeni ya Trump ilishirikiana na Urusi.

Wapelelezi wa Urusi wanaamini kwamba Urusi ilimsaidia bwana Trump kushinda uchaguzi wa mwaka jana kitu ambacho Urusi imekana.

Image caption Wakati wa mkutano huo wa chakula cha viongozi Bi Trump aliketi karibu na rais Vladmir Putin

Bwana Trump amepinga madai kama hayo.

Mkutano wa pili ulifanyika wakati wa chakula cha jioni cha viongozi katika kikao hicho cha G20 mjini Hamburg mapema mwezi huu

Rais wa Marekani alikuwa pekee na Putin alikuwa na mkalimani wake huku vyombo vya habari vya Marekani vikisema kuwa mkutano huo ulichukua saa moja.

Madai ya kilichozungumzwa yaliwasilishwa kwa maafisa wa Ikulu ya Whitehouse na bwana Trump mwenyewe kwa kuwa hakukuwa na wasaidizi wakati wa mkutano huo.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii