Msichana wa miaka 10 auwawa na simba Zimbabwe

Msichana wa miaka 10 auwawa na simba Zimbabwe Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msichana wa miaka 10 auwawa na simba Zimbabwe

Msichana wa umri wa miaka 10 ameuwawa na simba alipotoka nje usiku kwenda msalani nyumaa ya nyumba katika eneo moja lililo kijijii nchini Zimbabwe.

Shangazi wake Mitchell Mucheni, anadaiwa kutazama kwa mshangao jinsi simba huyo alivyomburuta msichana huyo kwenda kichakani.

Mwili wa msichana huyo ulipatikana karibu umbali wa mita 300 kutoka kwa nyumba yao.

Kisa hicho kinaripotiwa kutokea usiku wa Jumamosi.

Mada zinazohusiana