Nchi za kiarabu zaondoa orodha ya masharti 13 dhidi ya Qatar

Buildings are seen from across the water in Doha, Qatar (5 June 2017) Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Qatar imekataa masharti hayo

Mataifa manne ya kiarabu yanayoongozwa na Saudi Arabia sasa hayaishinikizi tena Qatar kutekeleza masharti 13 yaiyowasilishwa mwezi uliopita.

Wanadiplomasia kutoka nchini za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na Misri waliwaambia waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa kuwa sasa wanaitaka Qatar kukubali masharti sita makuu.

Hii ni pamoja na kujitoea kupambana na ugaidi na itikadi kali na kuchana na vitendo vya uchokozi.

Hakuna na tamko lolote kutoka kwa Qatar, ambayo inakana kuwaunga mkono magaidi.

Imekataa kukubali masharti yoyote yanayotishia uhuru wake au kuenda kinyume na sheria za kimataifa.

Vikwazo bva angani, ardhini na baharibi ilivyowekewa wiki sita zilizopita vimesababisha usumbufu katika taifa hilo la Ghuba, ambalo hutegemea kununua bidhaa kwa wakaazi wake.

Image caption Ramani

Mada zinazohusiana