Uruguay imekuwa nchi ya kwanza duniani kuhalalisha bangi

A man has his identity checked with a digital scanner before buying legal marijuana in a pharmacy in Montevideo, Uruguay July 19, 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uruguay imekuwa nchi kwanza duniani kuhalalisha mauzo ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha.

Uruguay imekuwa nchi kwanza duniani kuhalalisha mauzo ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha.

Maduka ya kuuza madawa 16 yalianza kuuza bangi leo Jumatano.

Karibu watu 5,000 wamejiandisha na serikali kuweza kununua bangi kwa njia halali.

Watanunua hadi gramu 10 kwa wiki na sio zaidi ya gramu 40 kwa mwezi.

Hatua hii inakuja miaka minne baada ya sheria kupitishwa iliyohalalisha biashara ya bangi.

Wale wanaounga mkono wanasema kuwa itasaidia kukomesha biashara haramu ya bangi na kuwatupa nje wauza madawa ya kulevya.

Wafanya biashara wanaweza kuchagua kutoka aina mbili ya bangi kati ya Alpha 1 na Beta 1.

Bei ya gramu tano za bangi itauzwa kwa dola 6.50

Bangi inayouzwa kwenye maduka ya mdawa hutoka mashamba yanayosimiwa na serikali.

Sheria hiyo pia huwaruhusu watu kupanda bangi yao nyumbani au kujiunga na vilabu vinavyofanya kilimo cha mmea huo.

Mada zinazohusiana