Kijana aliyepandikizwa mikono mipya Marekani

Zion Harvey Haki miliki ya picha Children’s Hospital of Philadelphia
Image caption Zion Harvey akicheza akitumia mikono mipya

Kijana wa kiume nchini Marekani ameweka historia kwa kuwa mtoto wa kwanza kupandikizwa mikono na kuweza kucheza ipasavyo mpira wa besiboli.

Ni miaka miwili tangu Zion Harvey ambaye sasa ana umri wa miaka 10, kupandikizwa mikono mipya, na madaktari wake wanasema kuwa wamefurahishwa na jinsi anavyoendelea.

Zion kwa sasa anaweza kuandika, kujilisha na pia kujivalisha nguo.

Licha ya mikono yake kutoka kwa mtu mwingine, ubongo wake umeikubali kama yake, kwa mujibu wa uchuanguzi uliofanywa.

Zion alizaliwa akiwa na mikono yote miwili lakini wakati alifikisha umri wa miaka miwili madaktari walilazimika kuikata.

"Wakati nilikuwa na umri wa miaka miwili, mikono yangu ilikatwa kwa sababu nilikuwa mgonjwa," alisema Zion.

Haki miliki ya picha Children’s Hospital of Philadelphia
Image caption Zion Harvey

Zion alikuwa na ugonjwa kwa jina sepsis, ambao ni hatari kwa maisha. Madaktari walikata mikono yake kwa sababu ilikuwa inakufa. Pia figo zake zilipata matatizo.

Akiwa na umri wa miaka minne, Zion aliwekewa figo kutoka kwa mama yake.

Upasuaji wa kumuwekea Zion mikono, uliofanywa mwezi Juni mwaka 2015 ulikuwa hatua kubwa.

Kando na uliofanywa mwaka 1998, wake Zion ulifanyiwa mtu mwenye umri mdogo zaidi.

Haki miliki ya picha Children’s Hospital of Philadelphia
Image caption Daktari mkuu Dr Scott Levin

Kundi wa watu 40 wakiwemo madaktari wa upasuaji 10, walimfanyia Zion upasuaji usiku wote hadi asubuhi kumpandikiza mikono yake mipya.

Changamoto kubwa waliyokumbana nayo ni kuunganisha mishipa midogo ya damu ambayo ingesaidia mikono yake kubaki kuwa hai.

Mada zinazohusiana