Rais Trump akutana na wabunge wa chama chake

Rais Donald Trump akutana na wabunge wa chama chake
Image caption Rais Donald Trump akutana na wabunge wa chama chake

Rais Donald Trump amekutana na maseneta wote 52 wa chama chake cha Republican na kuwataka kuupatia nguvu mpango wake ili uweze kuifuta sheria iliyo kuwepo ya huduma ya afya maarufu kama ObamaCare.

Rais huyo wa Marekani amewataka watunga sheria hao kutoondoka kwenda likizo ya mwezi wa Nane hadi pale watakapokubaliana mpango wa huduma ya afya ambao utaweza kupitishwa na mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

Wiki hii Rais Trump amekuwa akihaha baada ya wabunge wanne wa chama chake kusema kwamba hawataunga mkono muswada mpya wa sheria ambao unatarajiwa kuchukua nafasi ya ObamaCare.