Mahakama Marekani, yakataa ombi la Ikulu

Wanaharakati na mabango yao Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanaharakati na mabango yao

Mahakama kuu nchini Marekani imelikataa ombi la Ikulu ya nchi hiyo kuimarisha vikwazo vya safari kwa raia wa nchi sita za Kiislamu.

Majaji wa Mahakama hiyo wameunga mkono hukumu iliyotolewa na mahakama ya wilaya mji, Hawaii wiki iliyopita ya kuruhusu babu na ndugu wa karibu kutembelea familia zao zilizopo Marekani.

Lakini mahakama hiyo imeunga mkono amri ya utawala wa Rais Trump kuzuia wakimbizi kuingia nchini humo.

Toka Rais Trump aliposaini amri yake juu ya jambo hilo, suala hilo limekuwa likirudishwa nyuma na kupelekwa mbele kulingana na mfumo wa sheria wa Marekani.