Mali za Lula da Silva zashikiliwa

Lula Da Silva Haki miliki ya picha AFP
Image caption Lula Da Silva

Jaji nchini Brazil ameagiza mali za Rais wa zamani wa nchi hiyo Luiz Inacio Lula da Silva kudhibitiwa, baada ya kupatikana na hatia ya rushwa.

Jaji Sergio Moro amesema kiasi cha dola za Marekani laki mbili zimegunduliwa katika akaunti ya kiongozi huyo wa zamani.

Majengo matatu ya ghorofa kipande cha ardhi na magari mawili pia yanashikiliwa kufuatia amri hiyo iliyotolewa.

.

Bwana Lula ambaye alipata umaarufu wa uongozi nchini humo ataendelea kutumia mali zake, lakini iwapo rufaa aliyokata kupinga kifungo cha miaka tisa gerezani alichohukumiwa, itashindwa, mali hizo,zita kamatwa.

Mwenyewe amekuwa akidai kuwa mashtaka dhidi yake yamehamasishwa kisiasa.