Majeshi ya Cameroon tuhumani

Ramani ya Cameroon Haki miliki ya picha Atlas
Image caption Ramani ya Cameroon

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limedai kwamba majeshi ya Ulinzi ya Cameroon yamewatesa na kuwaua watuhumiwa kadhaa wanachama wa kundi lenye siasa kali la Boko Haramu.

Ripoti hiyo imesema miongoni mwa wanaoshikiliwa ni wanawake na watoto.

Shirika hilo la Haki za Binadamu limesema limetoa ushahidi wa madai ya uhalifu wa kivita kwa serikali ya Cameroon, lakini halikupata majibu yoyote.

Eneo la kaskazini mwa Cameroon na mataifa ya jirani kwa miaka kadhaa limekuwa likiharibiwa na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya usalama na wapiganaji wa Boko Haramu.