Udukuzi wa uchaguzi wa Marekani: Familia ya Trump yachunguzwa

Donald Trump jr, Jared Kushner na meneja wa kampeni za Trump Paul Manafort Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump jr, Jared Kushner na meneja wa kampeni za Trump Paul Manafort

Mwanawe mkubwa rais Donald Trump, aliyekuwa meneja wa kampeni pamoja na mkwe wake wanatarajiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati za bunge la senate zinazochunguza madai kuwa Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.

Donald Trump Junior na Paul Manafort wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge la senate ya haki siku ya Jumatano naye Jared Kushner anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya bunge hilo la intelijensia siku ya Jumatatu.

Watatu hao wametuhumiwa kuwa na uhusiano wa karibu na maafisa wa serikali ya Urusi.

Mapema mwezi huu Donald Trump Junior alichapisha barua pepe ambazo alionekana kukubali usaidizi kutoka kwa serikali ya Urusi, kuumpa nyaraka ambazo zingemuharibia Bi Hillary Clinton kampeni yake.

Rais Trump na washirika wake wamekana kufanya makosa yoyote.

Wakati huohuo Trump amesema kuwa asingemteua Jeff Sessions kuongoza uchunguzi huo iwapo angelijua kwamba anegjiondoa.

Katika Mahojiano na gazeti la New York Times , bwana Trump alitaja hatua hiyo ya mwanasheria mkuu kuwa isio ya haki.

''Sessions asingejitoa na iwapo angejitoa ,angeniambia kabla ya kukubali kazi hiyo na ningemchagua mtu mwengine'', alisema Trump.

Bwana Sessions alijiondoa katika usimamizi wa uchunguzi unaoituhumu Urusi kuingilia uchaguzi wa Urais na kumsaidia bwana Trump kushinda baada ya kukataa katika mahojiano kwamba alikutana na balozi wa Urusi nchini Mrekani.

Bwana Sessions hajatoa tamko lolote kuhusu matamshi hayo ya rais Trump