Korea Kusini yataka mazungumzo na Korea Kaskazini

Rais wa Korea Kusini Moon Jae in
Image caption Rais wa Korea Kusini Moon Jae in

Korea Kusini inasema kuwa imejiandaa kufanya mazungumzo ya kijeshi na jirani wake wa Korea Kaskazini , ijapokuwa Pyongyang bado haijatoa jibu lolote kuhusu wito huo ili kuanza mazungumzo mapema siku ya Ijumaa.

Uhariri wa gazeti kuu la Korea Kaskazini umesema ni upuzi mkubwa kwa Korea Kusini kupigania uhusiano mwema huku ikishikilia sera ya chuki dhidi ya Korea Kaskazini.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alipendekeza mazungumzo hayo ya ana kwa ana miaka mitatu iliopita ili kupunguza hali ya wasiwasi katika mpaka wa mataifa hayo.

Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong un

Seoul pia imesema kuwa inatazama kwa karibu ishara zozote za uchokozi za Korea Kaskazini huku kukiwa na ripoti kwamba PyongYang ilikuwa inajiandaa kufanyia majaribio kombora jingine la masafa marefu.