Mali ya waziri wa zamani wa mafuta nchini Nigeria yatwaliwa

Diezani Alison-Madueke

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Diezani Alison-Madueke

Mahakama nchini Nigeria imeamrisha kutwaliwa kwa muda mali ya thamani ya dola milioni 37.5, yanayomilikiwa na aliyekuwa waziri wa mafuta Diezani Alison-Madueke, kwa madai kuwa ilinunuliwa kwa pesa zilizopatikana kwa njia isiyo halali

Kutwaliwa kwa mali hiyo ni sehemu ya msururu wa kesi zilizowasilishwa na shirika la kupambana na ufisadi nchini Nigeria.

Shirika la AFP linasema kuwa mali hiyo ni nyumba iliyo katika eneo la Banana Island mjini Lagos.

Bi Alison-Madueke yuko mjini London ambapo ameachiliwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kutokana na madai ya ufisadi.

Alihudumu kama waziri wa mafuta chini ya uongozi wake Rais Goodluck Jonathan kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.