Mgomo wasababisha ghasia kali Venezuela

Waandamaaji wa walikabiliana katika miji kadhaa ya Venezuela

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Waandamaaji wa walikabiliana katika miji kadhaa ya Venezuela

Mamilioni ya Wavenezuela wameitikia wito wa Upinzani wa kubakia nyumbani, katika mgomo wa kwanza wa saa 24 kufanyika nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Hatua hiyo ni kupinga mipango ya serikali ya kuandika tena katiba mpya.

Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika miji kadhaa, walipopambana na waandamanaji.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Polisi walipambana na Waandamanaji

Katika ghasia hizo waandamanaji watatu waliuawa.

Hata hivyo, katika maeneo yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo mjini Caracas, maisha yaliendelea kama kawaida.

Katika hotuba yake kupitia televisheni, Rais Nicolas Maduro amesema mamia ya wafanyabiashara waliendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba viongozi wa mgomo huo watakamatwa.

Lakini upinzani nao umedai kuwa Rais Maduro anajaribu kujiimarisha madarakani kwa kubadili katiba, hali ambayo itabadili hali ya sasa ya upinzani kudhibiti bunge.

Na katika Umoja wa Mataifa mwanadiplomasia wa Venezuela amejiuzulu katika kupinga hatua zinazochukuliwa na serikali yake.