Harar: Mji wa Ethiopia ambao wakazi huishi na fisi

Harar: Mji wa Ethiopia ambao wakazi huishi na fisi

Mojawapo ya miji mikongwe zaidi nchini Ethiopia wiki hii imeadhimisha miaka elfu moja na kumi tangu kuanzishwa kwake. Maelfu ya watalii na wenyeji wamekuwa wakisheherekea katika mji huo wa Harar, Mashariki mwa Ethiopia. Mji huu pia hufahamika wakati mwingine nyingine kama Makka ya bara Afrika.

Mwaka wa 2006, Shirika la UNESCO lilitangaza mji huo kama Urithi wa Dunia.

Na kama mwanahabari wetu Emmanuel Igunza anavyoripoti, wenyeji wa Harar pia wana sifa ya kuwa na uhusiano wa kushangaza na wa kipekee na fisi wa mwituni.