Tamara amewezaje kuvuma katika Hip hop Tanzania?

Tamara amewezaje kuvuma katika Hip hop Tanzania?

Katika maeneo mengi barani Afrika idadi kubwa ya wanamuziki wa kufokafoka maarufu kama Hip hop huwa ni wanaume, lakini katika miaka ya hivi karibuni akina dada nchini Tanzania nao wanazidi kuchipuka katika aina hiyo ya muziki.

Tamara Ally Mohamed ni mmoja kati ya wanamuziki wachache wa kike wa muziki wa Hip hop ambaye mbali na kuwa ni mwanamke pia anatoka katika familia yenye msimamo mkali wa kidini.

Amewezaje kufanikiwa? Mwandishi wa BBC Munira Hussein alimuuliza Tamara swali hilo.