Wasichana wapewa baiskeli kuzuia mimba magharibi mwa Kenya

Wasichana wapewa baiskeli kuzuia mimba magharibi mwa Kenya

Tatizo la wasichana wadogo, hasa wale walio shuleni kushika mimba linazikumba jamii nyingi ulimwenguni.

Kenya ni mojawapo wa mataifa yanayojitahidi kukabiliana na janga hili na shule moja Magharibi mwa Kenya imejitokeza la suluhu ya kipekee - ambapo wanawapa wasichana baisikeli kwenda shuleni ili wasichangamane na watu wanaowaharibia maisha.

Mwenzetu Muliro Telewa alitembelea Shule ya Upili ya Lwanda katika Kaunti ya Kakamega, Magharibi mwa Kenya na kutuandalia taarifa ifuatayo.