''Trump anajaribu kujenga hadhi ya Urusi''

Aliyekuwa jasusi James Clapper
Maelezo ya picha,

Aliyekuwa jasusi James Clapper

Aliyekuwa mkurugenzi wa maswala ya kiinteligensia, James Clapper anasema wakati mwingine inaonekana kama raisi Trump anajaribu kuijenga Urusi kuwa taifa lenye hadhi kubwa tena.

Alikuwa akijibu swali alililoulizwa wakati wa kongamano la kiusalama lililofanyika huko Aspen,Colorado, iwapo Raisi Trump analipa uzito swala la uhusioano baina ya Marekani na Urusi.

Jenerali huyo mstaafu akajibu kua ilikua vigumu kuuleza bayana.

Jenerali Clapper ameongeza Urusi itakua daima ikifungamanishwa na jinsi ilivyo uathiri uchaguzi wa mwaka jana wa Marekani.