Rais wa Palestina akata mawasiliano na Israel

Rais Mahmoud Abbas
Maelezo ya picha,

Rais Mahmoud Abbas

Rais wa Palestinian , Mahmoud Abbas amekata mawasiliano na serikali ya Israel hivyo kuzidisha mzozo ambao umekuwa ukitokota wiki nzima kuhusu hatua kali zaidi zilizochukuliwa na Israel huko mji wa kale wa Jerusalem .

Wapalestina watatu walifariki hapo jana katika makabiliano makali na maafisa wa polisi wa Israeli katika eneo hilo.

Ghasia zilizuka pale polisi wa Israeli walipoweka vizuizi kuwazuia wanaume wote chini ya miaka 50 kushiriki salah ya Ijumaa katika msikiti wa Al-Aqsa eneo linalozozaniwa na pande hizo mbili kinzani.

Eneo hilo takatifu la ibada mjini Jerusalem, maarufu kama Hara al-Sharif, kwa waumini wa kislamu na Hekalu la mlimani kwa wayahudi.

Ripoti zaongeza kusema kuwa raia watatu wa Israel pia waliuawa katika mzozo huo huko eneo la ukingo mwa magharibi - West Bank