Raia wa East Timor kushiriki katika uchaguzi

East Timor kushiriki katika uchaguzi
Maelezo ya picha,

East Timor kushiriki katika uchaguzi

Karibu robo tatu ya wapiga kura millioni moja huko East Timor wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua wabunge sitini na tano.

Nchi hiyo iliokuwa koloni ya Ureno ilijipatia uhuru wake kutoka Indonesia miaka kumi na tano iliyopita.

Uchaguzi huo pia utamua nani atakua waziri mkuu wa nchi hiyo.

Wengi wa raia wa nchi hiyo wako chini ya umri wa miaka thelathini.

Serikali imeshutumiwa kwa kushindwa kutumia utajiri wa gesi na mafuta nchini ili kukuza nafasi za kazi hasa katika sekta ya nishati inayochangia asilimia tisini ya mapato ya serikali.