Manchester City yakubali kumnunua Benjamin Mendy

Beki wa kushoto Benjamini Mendy
Maelezo ya picha,

Beki wa kushoto Benjamini Mendy

Klabu ya Manchester City imekubali kumnunua beki wa kushoto wa Monaco Benjamin Mendy kwa kitita cha pauni milioni 52.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye alijiunga na Monaco kutoka Marseille msimu uliopita aliichezea klabu hiyo mara 34 msimu uliopita na kuisaidia kushinda taji la kwanza la ligi katika kipindi cha miaka 17.

Kitita hicho kitakipiku kile kilichotolewa na City kumnunua beki wa kulia Kyle Walker mapema mwezi huu pamoja na kile kilichotumiwa kumnunua John Stone msimu uliopita.

City haijathibitisha makubaliano hayo lakini inaamini kwamba kitita fulani kimekubaliwa.