Mwanamuziki Wizkid kutoka Nigeria atumbuiza Nairobi

Mwanamziki chipukizi wa Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kwa jina Wizkid, akitumuiza jijini Nairobi, Kenya
Maelezo ya picha,

Mwanamziki chipukizi wa Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kwa jina Wizkid, akitumuiza jijini Nairobi, Kenya

Mwanamziki chipukizi wa Nigeria, Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu kwa jina Wizkid amewatumbuiza zaidi ya mashabiki 3,000 jijini Nairobi, Kenya, usiku wa kuamkia Jumapili. Mwaandishi wa BBC Shaaban Ndege alikuwepo na ametuandalia taarifa ifuatayo.

Mashabiki walivumilia mvua na baridi kali usiku wa manane, pale muimbaji huyo alipoingia jukwaani akiporomosha magoma moto moto.

Maelezo ya picha,

Mashabiki waliovumilia mvua wakitumbuizwa na Wizkid

Maelezo ya picha,

Wizkid, akiwasisimua mashabiki wake mwishoni mwa juma Nairobi

Kabla ya kuingia jukwaani, wanamuziki wa Kenya, Redsan, Willy Paul, mwanadada Fena Jitu,Sauti Sol, FBI, Nameless mbali na wanamuziki wengine wa Kenya walitumbuiza.

Muimbaji chipukizi wa kike Gin Ideal hakuwafurahisha mashabiki, hatua iliyowafanya kumkemea akiwa jukwaani.

Muimbaji huyo wa muziki za ki-Nigeria na kimombo, alishabikikiwa na watu wengi waliomiminika katika uwanja wa Jumba la mikutano ya kimataifa- KICC Jijini Nairobi, kuhudhuria tumbuizo lake la amani nchini humo, siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya hapo Agosti 8 mwaka huu.

Maelezo ya picha,

Mwanamuziki wa kenya David Mathenge, maarufu kama Nameless akitumbuiza katika hafla hiyo

Wizkid ambaye siku 6 zilizopita, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, alzaliwa mnamo Julai 16 mwaka 1990 na aliingia katika ulingo wa muziki akiwa na umri wa miaka 11.

Mwaka 2009, alitia saini ya mkataba wa muziki na kampuni kubwa ya kurekodi muziki nchini Nigeria Banky W.'s, maarufu kwa jina Empire Mates Entertainment (E.M.E).

Aliinuka kimziki mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha mziki kwa jina "Holla at Your Boy" kabla ya kuchomoa album iitwayo Superstar (2011). "Tease Me/Bad Guys", "Don't Dull", "Love My Baby", "Pakurumo" and "Oluwa Lo Ni" ni baadhi ya muziki katika album hiyo ya Superstar.

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha,

Swabri Mohammed maarufu kwa jina Redson akiwa jukwaani

Albamu ya pili ya Wizkid - Ayo, ilirekodiwa Septemba 2014, ikiwa na magoma 6: "Jaiye Jaiye", "On Top Your Matter", "One Question", "Joy", "Bombay" na "Show You the Money".

Mwaka jana 2016, Wizkid alitambuliwa kimataifa baada ya kushirikiana na mwanamuziki wa Marekani Drake, alipochomoa kibao kikali, "One Dance", ambao ilichukua nafasi ya kwanza katika orodha ya miziki katika mataifa 15 duniani ikiwemo Marekani, Uingereza, Canada na Australia.

Maelezo ya picha,

Muimbaji chipukizi wa kike Gin Ideal akitumbuiza mashabiki

Mbali na kushirikiana na Drake, Balogun au Wizkid amechomoa vibao kadha shirika na wanamuziki kadhaa katika nyimbo "Girl" (na mwanamuziki Bracket), "Fine Lady" (na Lynxxx), "Sexy Mama" (na Iyanya), "Slow Down" (na R2Bees), "The Matter" (na Maleek Berry), "Pull Over" (na KCee) pamoja na "Bad Girl" (akishirikiana na Jesse Jagz).

Maelezo ya picha,

Mashabiki waliojazana KICC kwa tumbuizo hilo

Mnamo mwaka 2013, aliorodheshwa nambari 5 duniani na shirika la habari la Forbes pamoja na Channel O, katika orodha ya matajiri wa muziki barani Afrika.

Mwezi Februari 2014, Wizkid alikuwa mwanamuziki wa kwanza wa Nigeria kuwa na wafuasi milioni 1 katika mtandao wa kijamii wa Twitteer.r.