Upinzani wapanga migomo na uvunjaji sheria DRC kumuondoa kabila madarakani

Upinzani wapanga migomo na uvunjaji sheria DRC

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Upinzani wapanga migomo na uvunjaji sheria DRC

Upande wa upinzani katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, umetangaza mpango wa migomo na kuvunja sheria, kujaribu kumlazimisha Rais Joseph Kabila aondoke madarakani.

Mgomo wa jumla wa siku mbili utaanza tarehe 8 Agosti.

Maandamano ya pamoja yamepangwa kufanywa baadaye mwezi ujao, katika kila jimbo la nchi.

Katika taarifa yake, upinzani umesema, ikiwa Rais Kabila hato-taja siku ya uchaguzi ufikapo mwisho wa mwezi wa Septemba, basi watu waache kulipa kodi kwa serikali.

Muhula wa rais ulima-li-zika mwaka jana.

Makubaliano yaliyofikiwa baada ya Kanisa Katoliki kupatanisha, ni kwamba atabaki madarakani hadi Disemba mwaka huu, lakini rais baadae alisema, hakutoa ahadi yoyote.