BBC yaahidi kuondoa tofauti ya mishahara kati ya wanaume na wanawake

Chris Evans na Winkleman ndio wanalipwa zaidi upande wa wanaume na wananawake

Chanzo cha picha, PA/getty images

Maelezo ya picha,

Chris Evans na Winkleman ndio wanalipwa zaidi upande wa wanaume na wananawake

BBC imekiri kwamba inahitaji kufanya juhudi zaidi kuondoa tofauti za mishahara baina ya waanawake na wanaume.

Inasema kwa jumla mshahara wa wanaume, ni asilimia 10 zaidi ya wanawake katika shirika zima, na imeahidi kuondoa hitilafi hiyi ufikapo mwaka 2020.

Taarifa hiyo imetolewa kujibu barua iliyoandikwa na watangazaji maarufu wanawake, katika BBC, kumtumia mkurugenzi mkuu, Tony Hall, kumsihi aondoshe tofauti hiyo katika malipo.

Jumatano, BBC ilichapisha orodha ya watangazaji na waigizaji wake wanaopata karibu dola laki mbili kila mwaka kufuatana na maagizo ya serikali.

Katika orodha, thuluthi moja ni wanawake, na wanalipwa kidogo sana wakilinganishwa na wanaume.