Jeshi la Misri lawauwa wapiganaji nane wa IS

Miongoni mwa wapiganaji wa IS nchini Misri
Maelezo ya picha,

Miongoni mwa wapiganaji wa IS nchini Misri

Vikosi vya jeshi la nchini Misri vimesema kuwa vimewauwa washukiwa nane ambao ni wapiganaji wa IS Kaskazini mwa mji wa Cairo.

Wapiganaji hao walikua katika mazoezi yao ya kila siku sehemu iitwayo Fayoum.

Ni miongoni mwa kundi liitwalo Hasm ambalo lipo chini ya IS.

Liliibuka mwaka jana na tiyari limefanya mashambulizi kadhaa.