Jeshi la Nigeria lawauwa wanawake wa IS

Kundi la IS limeibuka kuwa tishio Nigeria
Maelezo ya picha,

Kundi la IS limeibuka kuwa tishio Nigeria

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limewauwa wanawake watatu ambao walikuwa akifanya jaribio la kulipua bomu kwa vikosi vilivyopo mji wa Borno.

Msemaji wa jeshi hilo Brogedia Jenerali Sani Usman amesema wanawake hao walionekana wakijaribu kuweka mtego ili kuvamia jeshi hilo karibu na mji wa Kawuri.

Kundi la kiislam la IS lilianzishwa katika mji wa Borno na tiyari limefanya mashambulizi kadhaa.