Shambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul

Smoke rising from the site of a car bomb attack in the western part of Kabul

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Shambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul

Shambulizi la bomu limesababisha karibu vifo vya watu 24 kwenye mji mkuu wa Afghanistan Kabul.

Kwa mujibu wa wizara ya ya mambo ya ndani nchini Afghanistan, takriban watu 42 pia walijeruhiwa wakati wa mlipuko huo.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika eneo lenye washia wengi magharibi mwa mji.

Lengo la shambulizi hilo halikutajwa mara moja na hakuna mtu aliyedai kuhusika.

Maelezo ya picha,

Shambulizi la bomu lawaua watu 24 Kabul

Shambulizi hilo llitokea karibu na nyumba na afisa wa cheo cha juu serikalini, Mohammad Mohaqiq.

Hakuna kundi la kigaidi lililodai kuhusika.

Mashambulizi ya awali yamedaiwa kutekelezwa na Taliban au kundi la Islamic State.

Kabul umekumbwa na misururu ya mashambulizi likiwemo lililowaua watu 90 wakati lori lililipuka mwezi Mei.