Asilimia 60 ya watoto China waliozaliwa mwaka huu ni wa pili

Asilimia 60 ya watoto China mwaka huu ni wa pili
Maelezo ya picha,

Asilimia 60 ya watoto China mwaka huu ni wa pili

Mamlaka kuu nchini China imetangaza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya zaidi ya watoto milioni saba waliozaliwa mwaka huu, ni watoto wa pili ambao familia zilikubaliwa kuzaa.

Hayo ni baada ya kibali cha sera ya kudhibiti idadi ya watu.

Sheria ya kuwaruhusu watu wanaoishi mijini kuzaa mtoto wa pili, ilimaliza mfumo uliodumu miongo kadhaa wa kuzitaka familia kuzaa mtoto mmoja pekee.

Hata hivyo, familia nyingi bado hazina haraka ya kuzaa mtoto wa pili, kwa sababu ya gharama kubwa ya masomo, inayoyumbisha juhudi za serikali ya kutaka kuongeza idadi ya watu, wenye nia ya kuwasaidia wazee ambao ni wengi sana nchini China.