Mkwe wa Trump akana kuwasiliana na maafisa wa Urusi

Mkwe wa Trump,jared Kushner akana kuwasiliana na maafisa wa Urusi
Maelezo ya picha,

Mkwe wa Trump,jared Kushner akana kuwasiliana na maafisa wa Urusi

Mkwe wa rais Donald Trump Jared Kushner ataliambia jopo la seneti baadaye kwamba sio yeye wala mwanachama yeyote wa kampeni ya Trump alishirikiana na maafisa wa Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani.

Atasema kwamba hakuwa na mawasiliano na kwamba hakutegemea ufadhili wa Urusi kuendesha biashara zake.

Bwana Kushner alitoa hotuba yake kabla ya mkutano huo.

Bunge la Seneti ,ikulu ya Whitehouse pamoja na wakili maalum wanachunguza uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi huo.

Bwana Kushner mwenye umri wa miaka 36 ni mshauri mwandamizi wa rais na alikuwa akisimamia kampeni ya Trump kuhusu maswala ya mipango ya kidijitali.

Amemuoa mwana wa Trump Ivanka.

Kushner ambaye hufanya mambo yake kwa usiri mkubwa atahudhuria kikao cha kamati ya upepelzi katika bunge la seneti kabla ya kuwasili mbele ya bunge la Congress siku ya Jumanne.

Katika taarifa hiyo aliyotoa siku ya Jumatatu, anasema: Sikushirikiana wala sijui mtu yeyote aliyejihusisha na serikali yoyote ya kigeni.

Maelezo ya picha,

Jared Kushner na Ivanka Trump

''Kuhusu mawasiliano na Urusi ama mwakilishi wa Urusi wakati wa kampeni'' ,hakuna alisema.

Mwisho wa taarifa hiyo anazungumzia kuhusu kumiliki anwani za watu wanne wanaowakilisha Urusi wote ikiwa wakati wa kampeni na baadaye.

Alikuwa akizungumzia mkutano na wakili wa Urusi Natalia Veselnitskaya mnamo mwezi Juni mwaka uliopita.

Wakili huyo alikuwa amemuahidi habari ambayo ingemuharibia jina Hillary Clinton.

Bwana Kushner alisema kuwa aliwasili kuchelewa katika mkutano huo na akagundua kwamba kulikuwa hakuna cha mno kilichokuwa kikizungumziwa.