Mtoto aliyezaliwa akiwa na HIV aishi miaka tisa bila virusi hivyo

Wanasayansi kutoka Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya HIV ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Chanzo cha picha, ManoAfrica

Maelezo ya picha,

Wanasayansi kutoka Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya HIV ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Wanasayansi kutoka Afrika Kusini wamebaini kwamba mtoto aliyeambukizwa virusi vya HIV ameishi kwa miaka minane na nusu bila viini hivyo.

Mtoto huyo alipewa dawa za majaribio ya kukabiliana na virusi hivyo alipokuwa mdogo lakini hajapewa dawa zozote za kukabiliana na HIV tangu aingie mwaka mmoja.

Hii ni mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa na virusi vya HIV kuweza kuishi bila virusi hivyo barani Afrika.

Wanasayansi waliogundua kisa hicho kwa sasa wanalinda utambuzi wa mtoto huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 9 na nusu.

Wanasema kuwa visa kama hivyo ni vichache na kwamba famili ya mtoto hyo ina furaha.

Dawa hiyo alipewa mtoto huyo wakati ambapo haikuwa swala la kawaida.

Watafiti wanaamini kupotea huko kwa vurusi sio kwa sababu ya matibabu ,lakini mtoto huyo ana jeni ama kinga isiyokuwa ya kawaida ambazo zimemlinda dhidi ya HIV.