Kiranja wa upinzani bungeni ashtakiwa na uchochezi Tanzania

Kiranja wa upinzani bungeni Tundu LIssu ashtakiwa na uasi Tanzania
Maelezo ya picha,

Kiranja wa upinzani bungeni Tundu LIssu ashtakiwa na uasi Tanzania

Kiranja wa upinzani bungeni nchini Tanzania Tundu Lissu ameshtakiwa na matamshi ya uchochezi

Katika mashtaka hayo mahakama iliambiwa kwamba mbunge huyo alitoa matamshi ya uasi dhidi ya serikali mnamo mwezi Julai 17 katika barabara ya Ufipa wilayani Kinondoni.

Mahakama iliambiwa kwamba taarifa hiyo ililenga kusambaza chuki dhidi ya serikali.

Wakati alipotakiwa kukana ama kukubali mashtaka hayo na jaji wa mahakama hiyo, Lissu alijibu kwamba hajafanya uhalifu wowote.

Kwa sasa upande wa mashtaka umeitaka mahakama kutomuachilia kwa dhamana huku wakili wa Lissu akitaka kiongozi huyo kuachiliwa kwa dhamana kwa kuwa ni haki yake ya kikatiba.

Mahakama hiyo itatoa uamuzi kuhusi dhamana hiyo siku ya Alhamisi.