Beki Eric Bailey aongezewa marufuku ya mechi 2

Eric Bailey wa Manchester United baada ya kupewa kadi nyekundu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eric Bailey wa Manchester United baada ya kupewa kadi nyekundu

Beki wa Manchester United Eric Bailey amepewa marufuku ya mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu dhidi ya Celta Vigo katika ligi ya Yuropa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alipewa kadi nyekundu katika nusu fainali ya mwezi Mei tarehe 11 na kukosa fainali dhidi ya Ajax, ambayo United ilishinda 2-0.

Hatahivyo marufuku hiyo sasa imeongezwa na itashirikisha mechi mbili.

Bailey atakosa mechi ya kombe la Supercup dhidi ya Real Madrid tarehe 8 mwezi Agosti na mechi United katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Kesi ya mchezaji huyo wa Ivory Coast haiwezi kumwezesha kukata rufaa kwa sababu soka ya Ulaya haiwezi kubadilisha uamuzi wowote usipokuwa ule ambao ulifanywa kimakosa.