Ureno yamtaka mtuhumiwa wa Italia

Ureno

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eneo la kihistoria lililolipuliwa mwaka 1974

Mahakama moja nchini Ureno wameamuru raia moja wa nchini Italia arejeshwe nchini mwake ambaye anatuhumiwa kuhusika na shambulizi la bomu mnamo mwaka 1974, ambalo liliua watu nane.

Shambulio hilo la bomu lilitekelezwa mjini Brescia, ambalo liliwaacha watu wapatao mia moja wakiwa majeruhi, ambao walikusanyika katika mkutano wa hadhara ambao walikuwa wakiupinga utawala wa kinazi katika uwanja mkubwa wa mikutano mjini humo.

Maurizio Tramonte, ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo nchini Italia cha maisha jela, alikamatwa tena mwezi June katika mji mkuu wa Ureno, Fatima, ambako alichukuliwa mateka.

Tramonte alihusishwa katika shambulizi hili la bomu baada ya kupokea amri kutoka kwa mwanachama mmoja Carlo Maria Maggi, wa kikundi fulani ambaye sasa ana umri wa miaka themanini na mbili ambapo yeye hatumikii kifungo kutokana na hali ya afya yake kuwa mbaya.

Bomu hilo la Brescia ni miongoni mwa mashambulio mengine yaliyotekelezwa na kikundi hicho chenye mrengo wa kulia mnamo mwaka ya 1970 na miaka ya 80, ikiwemo kituo cha treni cha Bologna ambapo watu themanini na tano walipoteza maisha.