Jared Kushner akana tuhuma dhidi yake

Marekani

Chanzo cha picha, Mary Evans Picture Library

Maelezo ya picha,

Mkwe wa Raisi wa Marekani Jared Kushner

Mkwe wa Raisi wa Marekani Donald Trump ambaye ni mshauri wake wa karibu, Jared Kushner, amelieleza jopo lenye kufanya uchunguzi wa kina ilikubaini kwamba anahusika katika kampeni chafu dhidi ya Urusi katika udukuzi wa kura uliosababisha kumuweka madarakani Raisi wa Marekani katika uchaguzi ulio fanyika mwaka jana.

Katika tamko lake la kwanza mbele ya vyombo vya habari wakati akijibu tuhuma hizo, bwana Kushner amesisitiza kwamba hahusiki na tuhuma za namna yoyote katika mawasiliano yake na wawakilishi wa serikali ya Urusi.

Ameeleza kwamba hajawahi kujihusisha kwa namna yoyote na misaada ya kifedha kutoka nchini kwa kufadhili biashara zake.

Kushner ametumia fursa hiyo kuwalaumu viongozi nchini mwake kwa kushindwa kuweka bayana mikutano yake na viongozi wa Urusi kwa vyombo vya ulinzi vya nchini Marekani.