China kuzindua mtandao usiodukuliwa

Chanzo cha picha, SPL
Teknolojia ya Quantum
Huku wadukuzi wakiendelea kushambulia mitandao kwa kutumia njia mpya, China inakaribia kuzindua mtandao ambao hauwezi kudukuliwa huku ukigundua shambulio lolote kabla ya kufanyika.
Teknolojia hiyo imebainika ni ile ya Quantum Cryptography, ambayo ni programu tofauti na ile inayotumika sasa ya Encryption na hutumia mwangaza kutuma habari muhimu.
Mradi huo wa China katika mji wa Jinan umetajwa kuwa hatua kubwa na vyombo vya habari nchini humo.
Mradi huo wa kwanza unatarajiwa kuweka historia kwa kuwa China inaongoza katika sekta ya kiteknolojia ambapo mataifa ya magharibi yamekuwa yakisitasita kuwekeza.
Katika mtandao huo watumiaji 200 kutoka Jeshi, serikali, idara ya fedha na sekta za umeme wataweza kutuma ujumbe ambao ni wao tu wanaoweza kuusoma.
Hatua hiyo ya China inamaanisha kwamba taifa hilo linapiga hatua kubwa katika kuimarisha programu ambazo zinaweza kulinda mtandao ambao ni rahisi kuushambuliwa kwa sasa.
Programu ambazo mataifa mengine huenda yakaanza kuzinunua kutoka kwa China.
Lakini ni teknolojia gani ambayo China imewekeza fedha nyingi kuimarisha?.
Iwapo unatuma ujumbe unataka uwe salama kutoka kwa wadukuzi, kwa sasa mbinu ya encryption ambayo inatumika sana inafanya kazi kwa kuficha neno la siri ambalo hutumika kusoma ujumbe huo katika mfumo mgumu wa hesabati.
Uimarishaji wa kompyuta unamaanisha kwamba nambari zinazotumika hulazimika kuongezwa urefu mara kwa mara.
Mbinu hiyo ya Encryption ina maisha mafupi na inaendelea kushambuliwa.
Kuna hofu kwamba utengenezaji wa kompyuta zenye programu hiyo ya quantum swala ambalo linaonyesha hatua kubwa zilizopigwa kunaweza kuziweka kompyuta zinazotumia mtindo wa encryption kuwa rahisi kushambulia.
Chanzo cha picha, SPL
Teknolojia ya Quantu