Acacia ''yakataa'' kuilipa Tanzania $180b

Lori linalotumika kubeba madini

Chanzo cha picha, ACACIA MINING

Maelezo ya picha,

Lori linalotumika kubeba madini

Serikali ya Tanzania imesema kuwa kampuni ya kuchimba dhahabu yenye makao yake nchini Uingereza Acacia inadaiwa na walipa kodi dola bilioni 180 ,kama malipo ya adhabu na riba, kulingana na taarifa ya kampuni hiyo.

Takwimu hiyo ni kulingana na ufichuzi uliofanywa na tume mbili za rais kuhusu sekta ya uchimbaji madini.

Kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Awamy deni hilo linalodaiwa Acacia linasimamia mapato yaliopatikana ambayo hayakutajwa kutoka kwa migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi katika kipindi cha mwaka 2000 na 2017.

Ikijibu, Acacia imepinga madai hayo na kusema kuwa inatafuta njia mbadala

Uchunguzi uliofanywa na tume hizo za rais uliishutumu Acacia kwa kufanya operesheni zake kinyume cha sheria na kushindwa kulipa inachodaiwa.

Acacia ambayo ndio kampuni kubwa inayochimba madini nchini humo ,imesisitiza kuwa imekuwa ikitangaza mapato yake.

Katika mkutano wa hadhara siku ya Ijumaa rais John Magufuli alitishia kufunga migodi yote ya dhahabu nchini humo iwapo kampuni za kuchimba madini zitachelewa kufanya mazungumzo na serikali yake yanayolenga kutatua madai ya ukwepaji kodi.