Trump amtaja mwanasheria mkuu Jeff Sessions kuwa ''dhaifu''

Rais Trump na Jeff Sessions: Bwana Trump amesema kuwa mwanasheria mkuu Jess Sessions ni dhaifu
Maelezo ya picha,

Rais Trump na Jeff Sessions: Bwana Trump amesema kuwa mwanasheria mkuu Jess Sessions ni dhaifu

Rais Donald Trump amemshambulia kwa mara nyenginje tena mwanasheria wake mkuu huku kukiwa na ripoti kwamba anatafuta ushauri kuhusu uwezekano wa kumfuta kazi jenerali Jeff Sessions akimtaja kama aliye ''dhaifu''.

Shambulio lake la hivi karibuni katika mtandao wa Twitter linajiri kufuatia ripoti kwamba rais huyo anatafuta ushauri wa kumfuta kazi kiongozi huyo wa mashtaka.

Siku ya Jumatatu alimtaja bwana Sessions kama asiye na ''uwezo wowote''.

Bwana Trump amesema waziwazi kwamba hafurahii hatua ya Sessions kujiondoa katika uchunguzi wa FBI kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani 2016.

''Mwanasheria Sessions amechukua msimamo dhaifu dhidi ya uhalifu uliotekelezwa na Hillary Clinton ambapo kuna barua pepe na huduma za DNC na vifichuaji vya Intel!''

Bwana Trump alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter siku ya Jumanne.

Mapema alihoji katika chapisho jingine kwa nini Sessions alikuwa haangazii ripoti mapema mwaka huu kwamba maafisa nchini Ukraine walitaka kushawishi uchaguzi wa mwaka uliopita nchini Marekani kumpendelea rais Trump dhidi ya Hillary Clinton.

Gazeti la Washington post limeripoti kwamba bwana Trump ametaka ushauri wa athari za kumfuta kazi bwana Sessions katika vyombo vya habari vya kihafidhina.