Meli ya Marekani yaionya ile ya Iran

Meli ya Marekani USS Thunderbolt

Chanzo cha picha, EPA/US DEPARTMENT OF DEFENSE

Maelezo ya picha,

Meli ya Marekani USS Thunderbolt

Maafisa wa ulinzi wa Marekani wamesema kuwa meli ya kivita ya Marekani imefyatulia risasi kadhaa meli ya Iran katika Ghuba.

Meli hiyo ijulikanayo kama The USS Thunderbolt ilifyatulia meli ya Iran baada ya meli hiyo kukiuka mawasiliano ya radio.

Meli hiyo ya Iran inayosemekana kusimamiwa na kikosi maalumu cha kijeshi nchini - Iranian Revolutionary Guard - ilikuwa ikienda kwa kasi na ikafika mita 50 karibu na meli hiyo ya Marekani.

Hakuna habari zo zote zilizotolewa na Iran.